HabariMilele FmSwahili

Mkewa Rais Margeret Kenyatta afungua rasmi hospitali ya Mama na Watoto Makueni

Mkewe raia Margeret Kenyatta  ametoa wito kwa serikali za kaunti kuwekeza raslimali zaidi katika kukuza ujuzi wa wahudumu wa afya mashinani. Bi Kenyatta anasema wahudumu hao wanatekeleza wajibu muhimu wa kuafikia jitihada za serikali kuwawezesha wakenya wote kupata huduma bora za matibabu kila walipo kwa urahisi. Amesema hayo alipoongoza uzinduzi wa hospitali ya kina mama na watoto katika eneo la wote kaunti ya Makueni.

Akiongea kwenye hafla hiyo gavana wa Makueni Kivutha Kibwana amesema hospitali hiyo ambayo ujenzi wake uligharimu shilingi milioni 135 itatoa huduma maalum zikiwemo za upasuaji. Wagonjwa kutoka kaunti jirani za Machakos, Kajiado, Kitui na Nairobi pia watapokea huduma katika hospitali hiyo.

Show More

Related Articles