HabariMilele FmSwahili

Naibu jaji Mwilu apinga kujumuishwa wakili Khawar Qureshi katika kesi ya ufisadi dhidi yake

Jopo la majaji 5 limeanza kusikiliza kesi mahakakani iliyowasilishwa na naibu jaji mkuu Philomena Mwili kupinga kushtakiwa kwa tuhumuza na utumizi mbaya wa mamlaka. Hata hivyo mwili amepinga vikali kujumuishwa wakili kutoka uingereza Khawar Qureshi katika kesi ya ufisadi inayomkabli. Kupitia wakili James Orengo Mwilu anasema mkurugenzi wa mashtaka ya umma Noordin Hajji hana mamlaka kisheria kumteua wakili Qureshi kusimamia kesi hiyo. Orengo pia anadai wakili Qureshi hajakabidhiwa cheti rasmi cha kuhudumu nchini.

Mawakili wa upande wa mashtaka wakiongozwa na Dorcas Oduor amepinga kauli hiyo akidai mawakili wa mwili hawakufuata utaratibu wa sheria ikiwemo kuwasilisha baerua rasmi kuhusu pingamizi lao.

Majaji chacha Mwita William Musyoka Hellen Omondi Francis Tuiyot na Mumbi Ngugi watatoa mwelekeo wakati wowote sasa.

Show More

Related Articles