HabariMilele FmSwahili

Ada ya kuengesha magari ya kibinafsi jijini Nairobi yapunguzwa

Ada ya kuegesha magari ya kibinafsi jijini Nairobi sasa imepunguzwa kutoka shilingi 300 hadi 200. Hii ni baada ya bunge la kaunti ya Nairobi kupasisha mswada wa fedha wa mwaka wa 2018 unaopendekeza kuwapunguzia wakazi gharama ya kuegesha magari. Kiranja wa wachache Peter Imwatok amesema hatua hiyo itawanufaisha wafanyibiashara wadogo na pia kuongeza kiwango cha mapato ya kaunti kutokana na ada ya kuehesha magari. Kauli sawa imetolewa na mwenyekiti wa bajeti kaunti ya Nairobi Robert Mbatia akisema swala hatua hiyo itadhibiti hulka ya baadhi ya madereva kuwahonga maafisa wa kukusanya ada hiyo. Ada ya kuegesha magari jijini iliongezwa kutoka shilingi 140 hadi 300 mwaka wa 2013.

Show More

Related Articles