Swahili Videos

Qureshi, Murgor, Taib na Kihara wateuliwa kumsaidia Noordin

Mkurugenzi wa mashtaka ya umma Noordin Hajji sasa amemteua wakili mtajika Khawar Qureshi kushughulikia kesi kuu na ngumu kuhusu ufisadi, hususan ile kumhusu naibu jaji mkuu Philomena Mwilu.
Wakili Qureshi, kulingana na wasifu wake, ni mtaalamu wa sheria za kimataifa na masuala magumu ya kibiashara, na anatarajiwa kuhusika katika kukabili ufisadi wa hali ya juu serikalini.
Hajji ambaye amekuwa mbele ya kamati ya senate kuhusu sheria amedokeza kuwa alichukua hatua hiyo kutokana na kuwa wanasheria watajika pamoja na walio katika afisi yake hawako tayari kushughulikia kesi hiyo.
Majaji watano wanatarajiwa kuanza kusikiza ombi la Mwilu Alhamisi hii la kutaka kuzuia kesi dhidi yake.

Show More

Related Articles