HabariPilipili FmPilipili FM News

Noordin Haji Aapa Kuelekea Mahakamani Kupinga Uamuzi Wa Mahakama Ya Rufaa.

Mkurugenzi wa mashtaka ya umma Noordin Haji ametishia kuwasilisha kesi katika mahakama ya  rufaa  ya kupinga uamuzi wa mahakama kuu wa kudinda kumsimamisha kazi  mwenyekiti wa tume ya ardhi  Muhammed Swazuri katika kesi inayomkabili.

Haji amesema atawasilisha rufaa hiyo kufuatia upendeleo unaofanyiwa baadhi ya maafisa wa umma na maafisa wa serikali ambao wanahusishwa na kesi za ufisadi na uhalifu wa kiuchumi.

Aidha amesema kulingana na katiba  maafisa wa serikali wanaomiliki afisi kuu nchini wanafaa kusimamishwa kazi na  kung’atuliwa kutoka ofisini pindi tu wanapojihusisha na utumizi mbaya wa mali ya umma.

Show More

Related Articles