HabariPilipili FmPilipili FM News

Uteuzi Wa Wanafunzi watakaojiunga na shule za upili za Extra County Kufanyika Leo

Wanafunzi watakaojiunga na shule za upili za Extra County mwakani watateuliwa leo katika zoezi litakaloendeshwa katika maeneo mbali mbali nchini.

Jumla ya wanafunzi 128,838 wanatarajiwa kujiunga na shule 540 za Extra-County nchini.

Wanafunzi  wengine 148, 215 watapa nafasi katika shule 1,030 za county ilhali 722,318 watajiunga na shule  7,085 za kaunti ndogo.

Kadhalika wanafunzi 1,626 watateuliwa kujiunga na shule 35 za wanafunzi wenye mahitaji maalum.

Waziri wa elimu balozi Amina Mohamed amethibitisha kuwa uteuzi huu utaendeshwa kieletroniki ili kuhakikisha usawa na wanafunzi wote kupokea barua zao kwa wakati.

Show More

Related Articles