HabariPilipili FmPilipili FM News

Idara Ya Usalama Yaanzisha Oparesheni Kali yakuwasaka Wahalifu Likoni.

Msako mkali unaendea huko likoni kuwasaka walanguzi wa dawa za kulevya, makundi ya vijana wanaohangaisha wakaazi pamoja na waliohusika kwenye uvamizi wa ofisi ya naibu kamishina gatuzi dogo la likoni.

Kamanda wa polisi kaunti ya Mombasa Johnston Ipara anasema msako huo hautasaza wahalifu na kuwa utaendelea hadi pale wahalifu wote watakapotiwa mbaroni.

Ipara aidha amewataka wananchi kushirikiana na maafisa wa usalama kutoa taarifa muhimu zitakazosaidia polisi kuwanasa wahalimu. Aidha anasema polisi wanashirikiana na viongozi wa nyanjani ili kuhakikisha hakuna wananchi atakayekamatwa kimakosa.

Show More

Related Articles