Swahili Videos

Baadhi ya wanafunzi walalamika kwa kutopata nafasi shule walizotaka

Maelfu ya wanafuzi jana walipokea barua zao za kujiunga na shule za kitaifa na zile za kaunti, kufuatia shughuli ya mchujo ya watahiniwa wa watakaojiunga na kidato cha kwanza zoezi la kidijitali ya kwanza humu nchini.
Kinyume na miaka ya hapo awali, sheria mpya za mchujo sasa zitashuhudia wanafunzi wakiwasilisha barua zao za kujiunga na shule ya upili kwenye mtandao .Zoezi ambalo linatarajiwa kuleta usawa na hata kukabiliana na visa vya ukora.
Itawabidi wanafunzi sasa kujiunga na shule walizochaguliwa kidijitali kwani ndio agizo la wizara ya elimu.

Show More

Related Articles