HabariPilipili FmPilipili FM News

Wakaazi Wa Ukunda Walalamikia Ongezeko La Nauli.

 

Wakaazi wa ukunda kaunti ya kwale wanalalamikia ongezeko la  nauli tangu kutolewa kwa agizo  kwa wahudumu wa gari za umma  kufuata sheria za trafiki  almaarufu sheria za michuki kikamilifu .

Wakiongozwa na  mwenyekiti wa wafanyibiashara eneo la ukunda  Richard onsongo  wanamesema kwamba nauli imeongezeka mara mbili ya ile ya  kawaida  kwani kutoka ukunda hadi  likoni ni shilingi 200 kinyume na hapo awali ambapo ilikuwa ni shilingi mia moja.

Aidha onsongo amesema kwamba anashangazwa na kupanda huko kwa nauli haswa ikizingatiwa kwamba bei ya mafuta haijapanda.

Show More

Related Articles