HabariMilele FmSwahili

Idara ya trafiki yapinga madai ya kusababisha msongamano wa magari jijini Nairobi

Idara ya trafiki imepinga madai maafisa wake ndio wanasababisha msongamano wa magari mjini Nairobi wakichukua hongo. Ni baada ya muungano wa oparesheni za matatu Nairobi,kudai kwa mwaka hupoteza shilingi milioni 24, kupitia hongo maafisa hao huchukua kutoka kwa wahudumu wa matatu. Mkuu wa trafiki nchini Samuel Kimaru akiyataja madia hayo kama propaganda zisizokuwa na ukweli.

Kimaru ameiambia Milele fm kwamba,muungano huo unatumia madia hayo kwa lengo la kususia kufuata sheria za trafiki, na kwamba hawatatishwa kwenye jukumu lao la kushughulikiai htrafiki

Show More

Related Articles