HabariPilipili FmPilipili FM News

Wanaohusika Na Uteuzi Wa Shule Za Upili Kwa Watoto Waliomaliza Darasa La Nane Kua Na Uwazi.

Wito umetolewa kwa maafisa wanaohusika na kuchagulia shule watoto watakaoingia kidato cha kwanza kuwa na uwazi wakati wa zoezi hilo.

Haya ni kwa mujibu wa naibu mwenyekiti wa chama cha walimu KNUT tawi la Kilindini Kombo Ahmed Kombo.

Kombo amesema kuna haja ya watoto watakaoteuliwa kwenda katika shule za kutwa kupata shule zilizoko karibu na maeneo wanayotoka ili kuwapa nafuu wazazi hasa wakati huu mgumu wa hali ya uchumi.

Amehoji kuwa kumpeleka mtoto shule ya mbali ni kumuongezea mzazi changamoto ya maisha.

 

Show More

Related Articles