HabariPilipili FmPilipili FM News

Idadi Ya Vijana Waliojitokeza Kwa Usajili Wa KDF Ya Pungua.

Idadi ya vijana walio jitokeza kwa usajili wa makurutu wa KDF mkomani eneo bunge la Nyali hii leo imetajwa kuwa ndogo  sana huku asilimia 90 ya vijana hao wakiwa  ni vijana kutoka maeneo mbalimbali na asilimia 10 pekee   wakiwa vijana kutoka eneobunge la Nyali.

Afisa  mkuu wa usajili wa makurutu hao JOSEPHAT  NZIOKA amesema hali hiyo ni kinyume na matarajio yake kwani ni mara yake ya kwanza kushuhudia idadi ndogo ya vijana eneo bunge hilo huku akiwasifia vijana hao waliojitokeza.

 

Show More

Related Articles