HabariPilipili FmPilipili FM News

Serikali Ya Kaunti Ya Nairobi Yafutili Marufuku Ya Magari Ya Umma Kuingia Katikati Mwa Mji Wa Nairobi.

Gavana wa Nairobi Mike Sonko amefutilia mbali marufuku ya magari ya usafiri wa umma kuingia katikati mwa jiji la Nairobi kwa muda.

Akiongea na wanahabari, Sonko amesema amechukuwa hatua hiyo ili kuendeleza mazungumzo na vyama vilivyathirika marufuku hiyo.

Amesema amezingatia pakubwa vilio vya wakaazi waliaothirika na marufuku hiyo.

Marufuku hiyo iliyoanza jana iliwaathiri maelfu wa wakaazi wa Nairobi ambao walilazimika kutembea kwa miguu kuelekea shughuli zao za kila siku.

Show More

Related Articles