HabariMilele FmSwahili

Luka Modric ashinda tuzo la Ballon d’Or

Kiungo wa Real Madrid na timu ya taifa la Croatia Luka Modric ameshinda tuzo la Ballon d’Or  mwaka 2018 Modric ndiye mchezaji wa kwanza tofauti na Lionel Messi na Cristiano Ronaldo kushinda tuzo hiyo baada ya miaka 10.

Modric 33, ameshinda kombe la Klabu Bingwa Ulaya mwezi Mei kwa mara ya tatu mfululizo na kulisaidia taifa lake kufika hatua ya fainali katika michuano ya Kombe la Dunia.

Mchezaji wa zamani wa Brazil na AC Milan Kaka, alishinda tuzo hiyo mwaka 2007, na baada ya hapo Messi na Ronaldo wameshinda mara tano kila mmoja tuzo hiyo ya thamani kabisa kwa wachezaji wa kandanda duniani.

Show More

Related Articles