HabariMilele FmSwahili

Wasafiri Nairobi walazimika kutembea mwendo mrefu kufuatia marufuku ya matatu kuingia jijini kuanza kutekelezwa

Maelfu ya abiria wamelazimika kutembea mwendo mrefu asubuhi hii kufuatia kuanza kutekelezwa marufuku kwa matatu kuingia kati kati ya jiji iliyowekwa na serikali ya kaunti. Maafisa wa polisi wameweka vizuizi bara barani na kuzizuia matatu. Hali hiyo imeshuhudiwa katika bara bara ya Thika ambapo matatu hazimeagizwa kusitosha safari zao katika kituo cha magari cha Ngara. Katika bara bara ya Jogoo polisi wanayazuia magari katika eneo la uwanja wa City ilhali katika bara bara ya Waiyaki matatu zimeelekezwa kwengineko katika eneo la Westlands. Ni hali inayotarajiwa kuzua mgogoro baina ya maafisa hao na wahuduu wa matatu wanaopinga marufuku hiyo.

Aidha abiria wengi walalamikia kulazimika kutembea mwendo mrefu kutokana na hatua hii.

Show More

Related Articles