HabariMilele FmSwahili

Wachina 3 wanaohusishwa na sakata ya tiketi za SGR kusalia korokoroni

Wachina watatu wanaohusishwa na sakata ya tiketi za SGR watasalia korokoroni mjini Mombasa baada ya kunyimwa dhamana na mahakama kuu ya Mombasa. Uamuzi wa kuwanyima dhamana 3 hao umetolewa na hakimu mkuu wa Mombasa Julius Nangea. Washukuwa wanakabiliwa na mashtaka ya kutoa hongo ya sh900,000 kwa maafisa wa DCI ili kuvuruga uchunguzi wa madai ya utapeli wa mauzo ya tiketi katika mradi wa SGR. Washukiwa hao watazuiliwa katika gereza la Shimo Latewa hadi disemba 10 ambapo kesi yao itasikilizwa.

Show More

Related Articles