HabariPilipili FmPilipili FM News

Wahudumu Wa Boda Boda Wahimizwa Kujiunga Na Vyama Vya Ushirika.

Wahudumu wa boda boda kwa mara nyingine wamehimizwa kujiunga na vyama vya ushirika yaani SACCOS hiyo ikiwa njia mojawapo ya kuwasaidia kujiwekea akiba.

Mwenyekiti wa chama cha SACCO cha waendeshaji bodaboda eneo la nyali hapa mombasa Samuel Ogutu amewataka wahudumu hao pia kutilia mkazo sheria za michuki ili kuzuia kujipata mikononi mwa serikali.

Kauli yake imetiliwa mkazo na naibu mwenyekiti Leornard Luvai ambaye amewataka waendeshaji wa pikipiki kujiunga na shule za mafunzo ya pikipiki ili kupata vibali halali.

Show More

Related Articles