HabariPilipili FmPilipili FM News

Twalib Abdalla Ameteuliwa Kuwa Afisa Mkuu Mtendaji wa EACC.

Tume ya maadili na kupambana na ufisadi nchini EACC imemteua aliyekuwa mwanajeshi Twalib Abdalla Mbarak kuwa afisa wake mpya mkuu mtendaji.

Mbarak anachukua nafasi ya Halakhe Waqo ambaye mda wake wa miaka 6 wa kuhudumu unakamilika hivi karibuni.

Mbarak aidha amepata nafasi hiyo baada ya kuwapiku wapinzani wake 13 waliokuwa wakiwania wadhfa huo, akiwemo Michael Mubea ambaye ni naibu afisa mkuu mtendaji wa tume hiyo.

Show More

Related Articles