HabariPilipili FmPilipili FM News

Bodi Ya Madaktari Imetakiwa Kutathmini Gharama Ya Matibabu Nchini.

Wizara ya afya nchini imeitaka bodi ya madaktari nchini kutathmini gharama ya matibabu nchini ili kusaidia katika kuafikia ajenda ya afya bora kwa wote.

Waziri wa afya Sicily Kariuki amedokeza kuwa bodi hiyo inafaa kuwajibika chini ya muda wa mwezi mmoja.

Ameitaka itoe ripoti itakayosawazisha gharama ya matibabu.

Kwa upande wake mwenyekiti wa kamati ya afya bungeni Sabina Chege ameweka wazi baadhi ya huduma za matibabu zilizoongezwa bei ikiwemo  upashaji tohara na kujifungua kwa kina mama.

Haya yanajiri miezi kadhaa baada ya tume ya EACC kutoa ripoti inayoashiria tofauti kubwa ya gharama ya matibabu wanayotozwa wakenya.

Show More

Related Articles