HabariMilele FmSwahili

Rubani ajeruhiwa baada ya ndege kuanguka Malindi

Rubani mmoja anaendelea kutibiwa baada ya kujeruhiwa  baada ya ndege alimokuwa  kuanguka  eneo la Furunzi mjini Malindi Kilifi. Meneja wa uwanja wa ndege wa Malindi Mohammed Karama anasema ndege hiyo ilipaa katika uwanja wa ndege huo ikiielekea mjini ukunda na ndipo ikaanguka muda mfupi baada ya kupaa. Mohammed anasema  ndege hiyo ilkua na rubani mmoja aliyekuwa mwanafunzi na ambaye alikua amehitimu urubani katika chuo cha Kenya School of Flying.

Show More

Related Articles