HabariPilipili FmPilipili FM News

Wakaazi Mombasa Wakinzana Na Utafiti Wa TIFA.

Siku moja baada ya utafiti wa kampuni ya TIFA kuorodhesha gavana wa Nairobi na mwenzake wa Mombasa miongoni mwa magavana walioimarisha utendakazi wao katika utoaji wa huduma, hisia mbalimbali zinaendelea kuibuka miongoni mwa wakazi katika kaunti za Nairobi na Mombasa.

Hapa Mombasa wakazi wameonekana kutoridhishwa na utafiti huo wengi wakilalamikia huduma duni hususan katika hospitali kuu ya Makadara, hata licha ya serikali kuwekeza kwa vifaa vya kisasa kushughulikia magonjwa sugu kama vile saratani na yale ya moyo.

Hata hivyo awali juma hili mbele ya kamati ya bunge gavana wa Mombasa Hassan Joho alitetea hali hiyo akisema kando na uwepo wa mashine za kisasa kunahitajika mafunzo maalum kwa Madakitari sawia na wataalam wa mashine hizo.

 

Show More

Related Articles