HabariPilipili FmPilipili FM News

Hatujachangia Kulemaza Utovu Wa Usalama Yasema Mashirika Ya Kijamii Pwani.

Mashirika ya kutetea haki za binadam kanda ya pwani yamekana madai kwamba yamechangia kulemeza juhudi za kuyakabili makundi ya uhalifu ambayo yamekuwa yakihangaisha wakazi kaunti ya mombasa.

Mahirika hayo yamekuwa yakilaumiwa kwa kuwatetea wahalifu pale wanapopigwa risasi na kuuawa na  maafsa wa polisi.

Hata hivyo akiongea na kituo hiki afisa wa dharura katika shirika la Muhuri Francis Auma amesema wao kama watetezi wa haki za binadam , hoja yao ni kupinga mauaji ya kiholela na wala sio kutetea wahalifu, akishikilia kuwa wahalifu wanapaswa kutiwa mbaroni na kupelekwa gerezani na wala sio kuuawa.

Auma Pia amepinga madai kwamba mashirika ya haki za binadam yanatumiwa na wafadhili wao kukashifu utendakazi wa polisi.

Show More

Related Articles