HabariPilipili FmPilipili FM News

Wanaotoa Leseni Kwa Wafanyibiashara Wa Vileo Kuchukuliwa Hatua Kali.

Idara ya polisi kaunti ya Taita-taveta imeonya kuwachukulia hatua kali wanaotoa  leseni kinyume cha sheria kwa wafanyibiashara wa vileo katika kaunti hiyo.

Kamishna wa kaunti hiyo Rhoda Onyancha anasema wengi wanaouza vileo wameanza kujihusisha na biashara haramu  ya dawa za kulevya.

Ameitaja hali hiyo kusababisha vijana wengi kujihusisha na utumizi wa dawa za kulevya na kuzorotesha hali ya usalama.

Tayari  gavana wa kaunti hiyo Granton Samboja ameanzisha operesheni kali dhidi ya pombe haramu ambayo imetajwa kukithiri katika jamii eneo hilo.

 

Show More

Related Articles