HabariPilipili FmPilipili FM News

Vikao Vya Kuupigia Kura Mswada Wa Thuluthi Mbili Huenda Vikahairishwa Kwa Kukosekana Idadi Ya Kutosha Ya Wabunge.

Wabunge hii leo wanatazamiwa kupiga kura zao  kuupasisha mswada wa thuluthi mbili ili kuwapa wanawake nafasi za kutosha za uwakilishi.

Hata hivyo kiongozi wa wengi bungeni Aden Duale na mwenzake wa wachache John Mbadi wanasema huenda shughuli hiyo ikaahirishwa kutokana na hofu ya kukosekana idadi hitajika ya wabunge kuupasisha mswada huo.

Wakati uo huo chama cha wabunge wa kike KEWOPA kimelionya bunge dhidi ya kufeli kupasisha mswada huo leo.

Mwenyekiti wa KEWOPA  Purity Ngirici na mbunge wa Kandara Alice Wahome wamesema huenda bunge likavunjiliwa mbali iwapo jaji mkuu David Maraga atamshawishi rais kufanya hivyo kwa kutoafikia matakwa ya katiba kuhusu uwakilishi sawa.

Show More

Related Articles