HabariMilele FmSwahili

Mahakama yamruhusu Jackie Maribe kurejea nyumbani kwake Lang’ata

Mwanahabari Jackie Maribie sasa amerejeshewa uhuru wa kuerejea katika nyumba yake iliyoko mtaani Royal Park  eneo la Lang’ata hapa nairobi. Maribe aliwasilisha kesi jana akidai kunyimwa kuingia nyumbani kwake licha ya kuachiliwa na mahakama Oktoba 30 katika kesi ya mauaji ya Monica Kimani inayomkabili. Katika idhini hiyo, upande wa mashtaka unasema umepata habari muhimu katika nyumba hiyo hivyo Maribe yuko huru kurejealea maisha yake. Hata hivyo upande huo kupitia Cathrene Mwaniki umekataa kumrejeshea Maribe simu yake ya rununu na gari lake kwa misingi bado zinatumika kama ushahidi wakati huu katika kesi ya mauaji ya Monica Kimani ikiendelea

Wakati huo mshukiwa mwenza na mpenzie Maribe,Jjoseph Irungu ameondoa kesi aliyowasilisha akitaka jaji wa mahakama  kuu James Wakiaga kuondolewa kusikiliza kesi ya mauaji inyaowakabili. Irungu alikuwa ameghadhabishwa na matamshi ya wakiaga aliyemuita jina la dharau ya woman eater sawa na male verson of a slay queen kutokana na miendeno yake ya maisha. Aidha mahakama imeridhia kilio cha Jowie anayedai kudhulimiwa katika gereza la kamiti anakozuiliwa na kuagiza alazwe katika hospitali ya KNH huku akiendelea na tiba yake ya jeraha ya risasii analouguza begani

Show More

Related Articles