HabariPilipili FmPilipili FM News

Watu Bilioni 2.5 Wanakabiliwa Na Changamoto Ya Mazingira Machafu Duniani Asema Rais Kenyatta.

Zaidi ya watu milioni 748 hawana maji safi na salama ya kunywa kote duniani.

Rais Uhuru Kenyatta akihutubia wajumbe wanaokutana Nairobi kwa siku ya pili kutoka mataifa 180 kujadiliana kuhusu utumizi bora wa bahari, anasema pia zaidi ya watu bilioni 2.5 wanakabiliwa na changamoto ya mazingira machafu kote duniani.

Hata hivyo rais Kenyatta anasema kuna faida nyingi zitokanazo na miji iliyokaribu na bahari,kama vile usafirishaji wa mizigo kutoka taifa moja hadi lingine kupitia bandari za mataifa hayo , na hivyo kuhimiza mataifa yenye bahari kuitunza vyema raslimali hiyo.

Kando na hayo  rais Kenyatta amehimiza ulimwengu kuweka mikakati ya kuzuia uchafuzi wa mazingira, sawia na kuweka mipango thabiti ya kuendeleza ukuaji wa miji kupitia miundo msingi ya kisasa bila kuongeza athari kwa mazingira.

Show More

Related Articles