HabariPilipili FmPilipili FM News

Wachina 3 Wanoakabiliwa Na Kesi Yakuuza Tiketi Za Magendo Kujua Leo Kama Wataachiliwa Kwa Dhamana Au La.

Raia watatu wa uchina waliopatikana wakijaribu kuwahonga maafisa wa DCI na shilingi laki tano ili kusitisha uchunguzi dhidi yao kuhusu kashfa ya kuuza tiketi za magendo katika kituo cha  SGR mjini  Mombasa kujua hatma yao leo endapo wataachiliwa kwa dhamana au la.

Watatu hao wamelazimika kukesha rumande katika gereza kuu la shimo la tewa hapa mombasa.

Aidha watatu hao wanadaiwa kujipatia mamilioni ya pesa kwa kuuza tiketi za gari moshi kwa njia za magendo katika kituo cha miritini.

Hakimu wa mahakama ya mombasa Julius Nang’ea aliyesikiza kesi hiyo jana, hii leo anatazamiwa kutoa siku ya kusikiza ombi la iwapo watatu hao wataachiliwa kwa dhamana au la.

Show More

Related Articles