HabariPilipili FmPilipili FM News

Wakuu Wa NHIF Kuridishwa Mahakamani.

Afisa mkuu wa shirika la bima ya kitaifa ya afya NHIF Geoffrey Mwangi na mkurugenzi wa fedha katika shirika hilo Wilbert Kurgat wanatarajiwa kurudishwa mahakamani leo.

Wawili hao wanakabiliwa na tuhuma za kukosa kushirikiana na maafisa wa jinai katika kuchunguza tuhuma za ufisadi katika shirika hilo.

Hapo jana hakimu Francis Abamani aliahirisha kesi ya wawili hao hadi hii leo, baada ya mawakili wa wawili hao wakiongozwa na Tom Ojienda kutaka ufafanuzi wa mashtaka yanayowakabili wawili hao, kwa madai kuwa mashtaka hayo hayakuwa wazi.

Kesi hiyo inatarajiwa kuendelea leo saa tanao ambapo Mwangi na Kurgat ‘watajua iwapo wataachiliwa kwa dhamana au la.

Show More

Related Articles