HabariPilipili FmPilipili FM News

Kongamano La Blue Economy Laingia Siku Ya Pili Nairobi.

Mkutano wa kimataifa kuhusu raslimali za bahari na vyanzo vya maji kama vile mito na ziwa almaarufu Blue Economy conference ,linaendelea kwa siku ya pili leo jijini Nairobi.

Hapo jana rais Uhuru Kenyata aliongoza marais wenzake  Mohamed Abdulahi wa Somalia, na Yoweri Museveni wa Uganda miongoni mwa wengine,  kutoa hotuba zao kwa wajumbe 11,000 wanaohudhuria kongamano hilo kutoka mataifa 180, wanaokutana kujadiliana jinsi ya kufanikisha maendeeleo kupitia raslimali za bahari.

Madhumuni ya mkutano huo ni kutathmini jinsi ya kuwekeza na kufaidi na raslimali za bahari, ikiwemo kuunda nafasi nyingi za ajira, kukuza uchumi wa mataifa mbalimbali, kuweka mkakati wa ushirikiano kwa mataifa yenye bahari na hata kujadiliana jinsi ya kuhifadhi vyanzo vya maji hususan bahari.

Show More

Related Articles