Swahili Videos

 MAMENEJA WA NHIF KIZIMBANI  : Mkurugenzi Mkuu na Mkurugenzi wa fedha kulala rumande hadi kesho

Wasimamizi wakuu wa hazina ya kitaifa ya bima ya kimatibabu NHIF, Geoffrey Mwangi na Wilbert Kurgat watasalia rumande kwa  siku nyingine moja, wakisubiri uamuzi wa hakimu mkuu Francis Andayi kuhusu mashtaka dhidi yao ya kuhujumu uchunguzi na kukaidi mahakama.
Wawili hao walifikishwa kortini mapema leo baada ya kukamatwa siku ya Ijumaa.
Kama mwanahabari wetu Grace Kuria anavyotueleza, idara ya upelelezi inachunguza madai kwamba baadhi ya wasimamizi wa NHIF huamuru  wafanyikazi katika hospitali mbalimbali nchini kuwapa hongo au kushiriki ngono nao ili walipwe fedha wanazopaswa kupata kutokana na wagonjwa wanaotumia kadi za NHIF.

Show More

Related Articles