HabariMilele FmSwahili

Majengo zaidi ya 3000 Nairobi yalijengwa bila kibali

Majengo zaidi ya 3000 hapa jijini Nairobi yamejengwa bila ya kupokea idhini. Katibu wa wizara ya ujenzi Profesa Paul Mariga amesema mengi ya majengo hayo yako katika mitaa ya Huruma Gachie na Githurai. Amesema misako imeimarishwa kuwanasa wamiliki wa majengo hayo yaliyo katika hatari ya kuporomoka. Pia amewaonya wanakandarasi kuwa watapokonywa lesini zao iwapo watapatikana na hatia ya kuhusika katika majengo hayo. Profesa Mariga pia ameshikilia kuwa jengo la Seefar hapa jijini Nairobi litabomolewa kama ilivyopangwa licha ya pingamizi kutoka wamiliki nyumba.

Show More

Related Articles