K24 TvNEWSSwahiliVideos

RAI MWILINI: Jinsi ya kutibu tatizo la kunuka miguu

Hali ya kunuka kwa miguu ni jambo ambalo huwafanya wengi kuona haya. Jambo ambalo wengi hawajui ni kuwa hali hii inaepukika.

Hali ya kunuka kwa miguu husababishwa na jasho jingi linalotokana na kuvaa viatu kwa muda mrefu na husababisha vimelea kumea kwenye miguu na uvundo mbaya .

Kutibu uvundo wa miguu.

1. Kata kucha.

2. Kausha maji katikati ya vidole baada ya kuoga.

3. Tumia soksi za kitambaa cha pamba badala ya kitambaa cha nailoni.

4. Osha viatu na dawa nje na ndani.

5. Toa viatu na sokisi ukiwa ndani ya nyumba

6. Kuwa na jozi kadhaa za viatu.

Show More

Related Articles