HabariPilipili FmPilipili FM News

Wanachama 47 Wa Kundi La MRC Washtakiwa Kwa Kosa La Kula Kiapo Kinyume Cha Sheria.

Watu 47 wanaoshukiwa kuwa wanachama wa kundi la MRC wamefikishwa katika mahakama kuu ya Mombasa mapema hii leo.

Wote hao wameshtakiwa na makosa ya kuandaa mkutano kinyume ya sheria, sawia na kulishwa kiapo kwa lengo la kuvuruga amani.

Washukiwa hao wanadaiwa kutekeleza hayo mnamo Novemba 22 katika maeneo ya Shelly beach Likoni kaunti ya mombasa, lakini wote wamekana mashaka dhidi yao, na kuachiliwa kwa dhamana ya shilingi laki moja kila mmoja au pesa taslimu shilingi elfu thelathini.

Kesi hiyo itatajwa tena tarehe 6 mwezi ujao wa disemba .

Show More

Related Articles