HabariPilipili FmPilipili FM News

Ripoti Ya KNEC Yaonyesha Wanaume Wachache Husomea Taaluma Ya Walimu Nchini.

Ripoti ya hivi karibuni inaonyesha kuwa wanaume wachache wanasomea taaluma ya walimu ikilinganishwa na wenzao wa kike.

Ripoti hiyo ya baraza la mitihani nchini KNEC inaonyesha kuwa kwa kipindi cha miaka 5 iliyopita , idadi kubwa ya waliofanya mtihani wa kozi ya walimu ni wanawake.

Ripoti hiyo aidha inaonyesha wanafunzi 17,879 wa kike walisajiliwa kwa kozi ya ualimu mwaka huu ikilinganishwa na wanafunzi 11,651 wa kiume.

Hali sawia ilishuhudiwa mwaka jana ambapo wanafunzi 13,646 wa kike walisajiliwa kwa kozi hiyo, ikilinganishwa na wanafunzi 10,402 wa kiume.

Show More

Related Articles