HabariPilipili FmPilipili FM News

Kisa Cha Kutekwa Nyara Kwa Raia Wa Italia Huenda Kikaathiri Sekta Ya Utalii Asema Owen Baya.

Serikali imetakiwa kufanya kila juhudi kuhakikisha mtalii Sylvia Constanca aliyetekwa nyara huko chakama kaunti ya kilifi anapatikana akiwa salama.

Akizungumza nje ya majengo ya Bunge, mbunge wa Kilifi Kaskazini Owen Baya amehofia kwamba huenda kisa cha utekaji nyara huo kikaathiri sekta ya utalii ambayo imeanza kunawiri katika eneo la pwani hususan miji ya kaunti ya Kilifi kama vile Malindi.

Baya pia ameitaka idara ya usalama kupunguza maafisa wake barabarani na badala yake kuwatuma katika sehemu zenye changamoto ya kiusalama ili kuimarisha doria.

Show More

Related Articles