HabariPilipili FmPilipili FM News

Kaunti Ya Kwale Kuwafadhili Wanafunzi Waliopita KCPE.

Kwa mara nyengine gavana wa Kwale Salim Mvurya ametoa hakikisho kwamba Serikali  yake itatoa ufadhili wa karo wa asilimia 100 kwa wanafunzi wote watakaojiunga na Shule za Upili za Kitaifa mwaka ujao.

Kauli yake inajiri siku chache baada ya kutangazwa matokeo ya mtihani wa kitaifa wa darasa la nane KCPE, ambapo wanafunzi wengi wa Kaunti ya Kwale wamenakili matokeo bora.

Mvurya amekariri kuwa Serikali ya Kaunti hiyo itawekeza zaidi katika sekta ya elimu, kama njia mojawapo ya kuinua hali ya uchumi na maendeleo ya wakazi wake.

 

Show More

Related Articles