HabariPilipili FmPilipili FM News

Visa 40,000 Vya Uvunjaji Sheria Barabarani Vimeripotiwa Asema Waziri Matiang’i .

Waziri wa usalama wa ndani Fred Matiang’i anasema serikali imeandikisha visa 40,000 vya uvunjaji wa sheria za barabarani  tangu zoezi la kukamata magari yasiyofata sheria za barabarani kuanza.

Matiang’ anasema zoezi hilo linaloendelea litaanza kuangazia wahudumu wa boda boda na TukTuk ili kuipiga msasa sekta hiyo ambayo imekuwa ikiandikisha idadi kubwa ya ajali na uhalifu mwengine nchini.

Waziri Matiang’ anasema  zoezi hili ni la kuhakikisha hakuna kisa hata kimoja cha vifo kutokana na ajali za  barabarani vitakavyo andikishwa hasa kwa   msimu huu wa likizo na sherehe za kufunga mwaka.

Show More

Related Articles