HabariPilipili FmPilipili FM News

Kauli Ya Mbunge Wa Kisauni Yapata Upinzani.

Shirika la kutetea haki za binadamu la MUHURI limeonyeshwa kughadhabishwa na kauli ya mbunge wa Kisauni Ali Mbogo kwa kile alichokitaja kuwa ni mashirika ya kijamii kuwatetea wahalifu katika jamii na kuwaacha wananchi wakiendelea kuangamia mikononi mwa majambazi.

Sasa mwenyekiti wa shirika la MUHURI Khelef Khalifa amemtaka Ali Mbogo kukoma kuingilia utendaji kazi wa mashirika ya kijamii badala  yake kushinikiza uwajibikaji wa polisi katika kukabiliana na wahalifu.

Kauli hii imeungwa mkono na mkurugenzi mkuu wa shirika la HAKI Afrika Hussein Khali anayesema katu mashirika ya kijamii hayasimami na wahalifu lakini yamekuwa mbioni kuhakikisha washukiwa wote wanapewa haki ya kisheria kabla ya kuchukuliwa hatua.

Show More

Related Articles