HabariMilele FmSwahili

Aukot ataka mageuzi ya katiba kutaja mauaji kiholela kuwa ukiukaji wa haki

Kiongozi wa chama cha Thirdway Alliance Dkt Ekuru Aukot sasa anaitaka serikali kubuni jopo maalum la mahakama kusaka mbinu za kutatua suala la kupotea watu na madai ya mauaji ya Kiholela nchini. Akizungumza mjini Mombasa katika mkutano ulioandaliwa na shirika la Haki Afrika dkt Aukot pia amependekeza mageuzi ya katiba kutaja mauaji ya Kiholela kuwa ukiukaji haki za kibidamau. Dkt Aukot amewasuta maafisa wa polisi nchini akisema wamefeli kuchunguza na kukabili mauaji hayo yaliyokothiri hasaa katika eneo la Pwani.

Show More

Related Articles