HabariMilele FmSwahili

Polisi wawasaka washukiwa waliomteka nyara  raia wa Italia Malindi

Maafisa wa usalama kwa ushirikiano na wale wa jeshi wanasaka genge la wahalifu wanaoaminika kuwa Al Shabab na ambao walimteka nyara raia wa Italiano anayeshirika huduma za kujitolea eneo la chakama kaunti ya Kilifi. Genge hilo pia limetekeleza mashambulizi na kuwajeruhi  watu 5 katika eneo hilo usiku wa kuamkia leo. Inadaiwa watu 8 waliojihami kwa silaha walivamia makao ya watoto yanayojulikana kama Afrika Milele katika kijiji cha Gaba na kutekeleza mashambulizi hayo.

Katika hospitali ya Malindi, manusura wa shambuliizi hilo wanaendelea kupokea matibabu. Walioshuhudia kisa hicho wakisema kilikuwa cha kuogofya

Huku taharuki ikitanda, wenyeji wanadai asasi za usalama eneo hilo Zimezembea.

Show More

Related Articles