HabariPilipili FmPilipili FM News

Ken Chonga Ahimiza Wazazi Kuwapa Elimu Watoto Wao Kilifi.

Mbunge wa Kilifi Kusini Ken Chonga amewataka wazazi katika kaunti ya kilifi kutunza na kuwapa elimu watoto wao ili waweze kupata nafasi nzuri za kazi katika serikali ya kitaifa.

Chonga amesema ni wakati wa wazazi kuwa mstari wa mbele kuleta maendeleo kupitia watoto wao badala ya kuwaachia viongozi na mashirika mbali mbali kulinda na kuelimisha mtoto.

Chonga amedai kwamba wazazi wengi wamekuwa wakilaumu watoto wao kutopewa nafasi za kazi katika serikali ya kaunti na ile ya kitaifa huku wakiwa ndio chanzo cha watoto kupotoka na kuzembea katika elimu.

Show More

Related Articles