HabariPilipili FmPilipili FM News

Raia Wa Italia Atekwa Nyara Eneo La Chakama Kilifi.

Watu wanaoshukiwa kuwa wanamgambo wa alshabaab wanadaiwa kuvamia kituo cha biashara cha Chakama kilomita kadhaa kutoka mjini Malindi mwendo wa saa mbili jana usiku.

Inadaiwa washukiwa hao walikuwa wamejihami kwa bunduki aina ya AK47.

Kulingana na taarifa ya polisi washukiwa hao walifanikiwa kuwajeruhi watu watano ambao kwa sasa wanaendelea kupokea matibabu.

Pia wamefanikiwa kumteka nyara mwanamke mmoja raia wa Italy ambaye anafanya kazi na shirika moja la NGO karibu na eneo hilo.

Kufikia sasa chanzo cha shambulizi hilo bado hakijabainika huku polisi wakiendeleza msako wa washukiwa hao.

Show More

Related Articles