HabariPilipili FmPilipili FM News

Uchumi Wataifa Watajwa Kuimarika Pakubwa.

Katibu mkuu katika wizara ya fedha Kamau Thuge amekanusha madai kwamba nchi hii haina uwezo wa kulipa deni inalodaiwa.

Akizungumza katika kongamano la wahasibu la ICPAK hapa Mombasa Thuge amesema kwa muda wa mwaka mmoja, uchumi umeimarika haswa katika sekta ya kilimo kwa asilimia 6 ,utalii ukiimarika kwa asilimia 5 na viwanda kwa asilimia 60, thibitisho kwamba taifa  lina uwezo wa kulipa madeni yake.

Kauli hii imeungwa mkono na naibu Mkurugenzi wa ICPAK Denis Osodo, ambaye amesema ipo haja ya  viongozi wa idara mbali mbali katika serikali, kutumia fedha kwa njia inayofaa ili kupunguza ubadhirifu wa mali ya umma.

Anasema pia kuna haja ya kuhamasisha  wananchi kulipa ushuru ili kusaidia katika kupunguza deni la taifa

Show More

Related Articles