HabariPilipili FmPilipili FM News

Walimu Wanaofunza Bila Kuhitimu Chuma Chao Ki Motoni.

Tahadhari imetolewa kwa walimu ambao wanahudumu bila mafunzo na vifaa ya ualimu kote nchi

Serikali imesema itaanzisha msako kote nchini wa kuwasaka walimu ambao hawana stakabadhi zinazohitajika katika taaluma ya ualimu.

Afisaa mkuu mtendaji wa TSC Nancy Macharia amsema serikali itawachukulia hatua za kinidhamu wakurugenzi ambao wana walimu ambao hawajahitimu kuhudumu kama walimu.

Wakati huo huo Nancy ametahadharisha shule  zinazowaajiri walimu waliotolewa kwenye sajili ya walimu kutokana na viwango duni vya maadili akisema hiyo inahatarisha maisha ya wanafunzi.

Show More

Related Articles