HabariPilipili FmPilipili FM News

Uwanja Wa Ndege Wa Moi Mjini Mombasa Kufanyiwa Ukarabati.

Serikali imezindua Ukarabati wa kiwanja cha ndege cha Moi international Airport utakao gharimu Dola milioni sabini ili kukipanua na kukiiimarisha kiwanja hicho katika kuvutia wawekezaji katika usafiri wa ndege.

Akizungumza katika uwanja Wa ndege wa Moi mjini Mombasa waziri wa uchukuzi James Macharia amesema ujenzi huo utafanikishwa kupitia ushirikiano Wa serikali na taifa la Ufaransa.

Upanuzi huo unatarajiwa kukamilika baada ya miaka miwili na kusaidia katika kuboresha huduma za kiwanja hicho cha ndege sawia na katika kubuni ajira zaidi.

Show More

Related Articles