HabariMilele FmSwahili

Maseneta kupiga kura kuhusu ripoti ya sakata ya ardhi ya Ruaraka leo

Maseneta leo wanatarajiwa kupiga kura kuhusu ripoti inayoshinikiza waziri wa usalama wa kitaifa dkt Fred Matiangi na katibu wa wizara ya elimu Belio Kipsang kuwajibikia sakata ya ardhi ya Ruaraka. Ripoti hiyo iliyoandaliwa na kamati ya seneti ya hesabu za umma na uwekezaji inapendekeza kuwa wawili hao waadhibiwe kwa madai ya kuruhusu malipo ya shilingi bilioni 1.5 ya ardhi hiyo ilikojengwa shule ya msingi ya drive in na ile ya upili ya Ruaraka.

Show More

Related Articles