HabariPilipili FmPilipili FM News

Kikosi Cha Kulinda Fukwe Za Maji Cha Zinduliwa Na Rais.

Hatimaye rais Uhuru Kenyatta amezindua rasmi kikosi cha kulinda fukwe za pwani ya kenya (kenya coast Guard) leo katika eneo la Liwatoni hapa Mombasa.

Pamoja na hayo rais wa nchi amezindua meli ya MV Doria yenye uwezo wa kukabili maadui wa baharini na yenye mwendo wa kasi zaidi.

Meli hiyo yenye mashine za kisasa ni ya kipekee katika nchi za Afrika.

Hatua hii itasaidia kupunguza mzozo uliokuwa ukishuhudiwa kwa wavuvi wa Kenya katika maeneo ya mipakani huku usalama wa majini wa taifa la kenya ukiimarika zaidi.

 

Akiongea baada ya zoezi la uzinduzi rais Kenyatta  ameelezea matumani ya kukomesha uhalifu wa baharini na kuimarisha uchumi wa nchi.

Show More

Related Articles