HabariMilele FmSwahili

Rais Kenyatta aongoza hafla ya kufuzu makurutu wa shirika la NYS Gilgil

Rais Uhuru Kenyatta amewaonya wanaopora mali ya shirikla ka huduma kwa vijana NYS kwamba hatawavumiliwa tena. Akizungumza baada ya kuongoza hafla ya kufuzu kwa makurutu elfu 16 wa shirika la NYS waliokuwa wakipokea mafunzo katika taasisi yao ya Gilgil, amesema wote waliopora mali ya NYS wataandamawa na mali hizo kurejeshwa.

Ametangaza serikali inatekeleza mageuzi kadhaa katika shirika la huduma kwa vijana nchini NYS. Rais amsema mabadiliko haya yatafanikisha utendakazi wake hata zaidi.

Rais amesema vijana hao watachangia pakubwa katika utekelezaji wa agenda zake nne kuu. Zaidi ya viiana elfu 16,000 wamefuzu kwenye hafkla ya leo.

Show More

Related Articles