HabariMilele FmSwahili

Watu zaidi ya 2000 wakamatwa kwa tuhuma za kukiuka sheria za trafiki

Watu zaidi ya 2000 wamekamatwa kwa tuhuma za kukiuka sheria za trafiki kufuatia msako ulioendeshwa katika bara bara kadhaa za mashariki mwa nchi. Kamanda wa polisi eneo la mashariki Moses Ombati amesema miongoni mwa waliokamatwa ni madereva 300 wa matatu ambao tayari wameshtakiwa mahakamani. Akihutubia wanahabari ofisini mwake Ombati amesema polisi pia wamefanikiwa kuwanasa wahudumu 280 wa boda boda. Hata hivyo amesema bado wanakabiliwa na changamoto ya ukosefu wa ushirikiano kutoka kwa umma katika kufanikisha utekezaji wa sheria za Michuki.

Huko Isiolo polisi wamekabiliana na wahudumu wa bodaboda walioandamana kupinga sheria za Michuki. Ni hali ambayo imewalazimu wenye maduka katika mji huo kufunga biashara zao.

Show More

Related Articles