HabariPilipili FmPilipili FM News

Achani Apiga Kampeni Yakukabili Mimba Za Mapema.

Naibu gavana kaunti ya Kwale Fatuma Achani ameanzisha kampeni  ya  kupambana na janga la mimba za mapema, ambalo linaonekana kukithiri katika kaunti za pwani miongoni mwa wasichana wa umri mdogo.

kampeni hiyo itahusisha makundi ya kinamama  kufanya hamasa katika jamii  kuhusu athari za mimba  za mapema kwa watoto wao wakike.

Kwa upande wao viongozi wa kidini hapa mombasa wakiongozwa na katibu mkuu wa baraza la maimamu na wahubiri nchini CIPK wametoa wito kwa jamii na hasa wazazi kupunguza uhuru mkubwa kwa watoto wao na kuhakikisha wanahudhuria madharasa  kupewa mafunzo ya kidini, wakisema hiyo ndio njia pekee itasaidia kuthibiti mimba za mapema.

Show More

Related Articles